• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kombe la Dunia, Bado siku 28: Hatimaye kocha mkuu wa Uingereza atangaza majina 30 ya awali

  (GMT+08:00) 2018-05-17 08:41:49

  Hatimaye kocha mkuu wa Uingereza Gareth Southgate ametangaza kikosi cha awali cha wachezaji watakaoshiriki kombe la dunia mwaka huu ambacho atakifanyia mchujo na hatimaye kubaki 23 ambao watatangazwa rasmi June 4.

  Katika uteuzi huo ameamua kuwatumia magolikipa wapya ambao ni Jack Butland (Stoke City), Jordan Pickford (Everton), Nick Pope (Burnley), jambo lililomfanya amwache Joe Hart, lakini pia kutokana na wingi wa vipaji Southgate amemuweka kwenye wachezaji wa akiba kiungo Adam Lallana wa Liverpool.

  Lakini kikosi kizima ni kama ifuatavyo,

  Walinzi ni Trent Alexander-Arnold (Liverpool), Gary Cahill (Chelsea), Fabian Delph (Manchester City), Phil Jones (Manchester United), Harry Maguire (Leicester City), Danny Rose (Tottenham Hotspur), John Stones (Manchester City), Kieran Trippier (Tottenham Hotspur), Kyle Walker (Manchester City), Ashley Young (Manchester United)

  Viungo ni Dele Alli (Tottenham Hotspur), Eric Dier (Tottenham Hotspur), Jordan Henderson (Liverpool), Jesse Lingard (Manchester United), Ruben Loftus-Cheek (Chelsea)

  na washambuliaji ni Harry Kane (Tottenham Hotspur), Marcus Rashford (Manchester United), Raheem Sterling (Manchester City), Jamie Vardy (Leicester City), Danny Welbeck (Arsenal).

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako