• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya:Kaunti ya Makueni yapewa sh milioni 110 za mradi wa maembe

    (GMT+08:00) 2018-05-17 18:10:03

    Muungano wa ulaya umeipatia kaunti ya Makueni shilingi milioni 110 kuboresha kiwanda cha kusindika na kutayarisha maji ya sharubeti kutoka kwa maembe.

    Kaunti hii itakuwa ya kwanza kunufaika kwa fedha za usaidizi za EU katika makubaliano ya kufadhili miradi kwenye kaunti 15 nchini Kenya.

    Zaidi ya familia elfu 12 katika kaunti hii zinatarajiwa kunufaika kiuchumi kwani bei ya kilo moja ya maembe inauzwa kwa shilingi 15.

    Stefano Dejak balozi wa EU nchini Kenya ameahidi kuimarisha maisha ya wakulima,kuongeza ajira na kuongeza mapato ya kaunti hiyo kupitia kwa matumizi bora ya fedha hizo.

    Kaunti ya Makueni inayoongozwa na gavana Profesa Kivutha Kibwana inalenga kuongeza mapato ya asilimia 40 kutoka kwa mradi huo pamoja na kuwapa wakaazi uhuru wa kiuchumi.

    Baadhi ya miradi itakayofanywa na fedha hizo ni utengenezaji wa masoko ya kisasa,mashine bora pamoja na vifaa vya usindikaji wa maembe na maziwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako