• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya:Kebs yaharibu bidhaa ghushi katika bandari ya Mombasa.

    (GMT+08:00) 2018-05-17 18:10:36

    Wafanyibiashara walioingiza mchele ulioharibika,spaghetti mbovu na magurudumu yaliyotumiwa kupitia bandari ya Mombasa wamepata hasara ya mamilioni ya pesa baada ya serikali kuziharibu bidhaa hizo.

    Shirika la ubora wa bidhaa nchini Kenya KEBS ,limeshtumu vikali wafanyibiashara hao walioingiza makasha 163 ya bidhaa hizo za thamani ya shilingi milioni 250.

    Meneja mkurugenzi Charles Ongwae amesema mchele huo ulipatikana umeoza wakati wa kununuliwa kabla ya kusafirirhswa na uko chini ya viwango vya utumiaji.

    Oparesheni kali ya uchunguzaji wa bidhaa zinazosafirishwa nchini Kenya imeanzishwa na shirika la ubora wa bidhaa pamoja na halmshauri ya ushuru ya kubainisha bidhaa na ulipaji ushuru.

    Waziri wa viwanda Adan Mohamed nae ameonya wafanyibiashara hao kufikishwa mahakami na kupewa adhabu kali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako