• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka, Golikipa Buffon kutangaza siku ya jumamosi, amuomba radhi refarii aliyemtolea lugha mbaya

    (GMT+08:00) 2018-05-18 08:57:12

    Golikipa wa kimataifa wa Italia Gianluigi Buffon ametangaza kuwa atatangaza hatma yake ya kustaafu soka siku ya mchezo wa mwisho wa klabu yake ya Juventus itakapocheza dhidi ya Hellas Verona jumamosi Ijayo.

    Buffon aliyasema hayo jana kwenye mkutano na waandihsi wa habari ambapo pia alitumia fursa hiyo kumuomba radhi mwamuzi Michael Oliver wa Uingereza kutokana na lugha aliyoitoa baada ya mwamuzi huyo kumuadhibu kwa kumpa kadi nyekundu kwenye mechi ya robo fainali ya klabu bingwa ulaya walipocheza dhidi Real Madrid.

    Buffon mwenye miaka 40 sasa, ameichezea klabu yake ya Juve mechi 508 tangu ajiunge nayo mwaka 2001, na kwa upande wa timu ya taifa amecheza mechi 176, lakini katika maisha yake ya soka Buffon amecheza jumla ya mechi 1050, akishinda ubingwa wa ligi kuu ya Italia mara 9, kombe la Italia mara 5, kombe la mataifa ya ulaya 1 na kombe la dunia mara 1.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako