• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkuu wa Jumba la makumbusho la China: Mawasiliano kati ya staarabu tofauti huakisi uundani wa kitamaduni wa vitu vya kale

    (GMT+08:00) 2018-05-18 13:59:14

    Leo tarehe 18, Mei ni Siku ya Kimataifa ya majumba ya Makumbusho, kauli mbiu kwa mwaka huu ni "majumba ya makumbusho yenye muunganiko mpana: mbinu mpya na umma mpya". Alipohojiwa na mwandishi wetu wa habari hapo jana, mkuu wa jumba la makumbusho la taifa la China Bw. Wang Chunfa alisema katika zama mpya, jumba hilo litafanya juhudi za kutumia mbinu mpya za muuganiko mpana kutambua thamani ya kitamaduni ya vitu vya kihistoria na kuboresha maisha ya kiroho ya umma.

    Bw. Wang Chunfa amesema msingi wa jumba la makumbusho ni maonyesho ya vitu vinavyohifadhiwa, na cha muhimu ni kutoa vitu vinavyoonyeshwa kwa umma ili kukidhi mahitaji yao yanayoongezeka.

    "Naona 'muunganiko mpana' unatutaka tuungane na umma na historia kwa pamoja. Jukumu la jumba la makumbusho ni kukusanya vitu vya kihistoria vyenye kumbukumbu na kuvionyesha kwa kutumia mbinu za kisasa. Pia tunapaswa kuungana na kuwasiliana na majumba mengine ya makumbusho, jumba moja haliwezi kukusanya vitu vyote vya kihistoria japokuwa ni kubwa na lina ushawishi mkubwa. Vilevile mbinu na njia ni muhimu katika kutimiza 'muunganiko mpana', na tunatumia teknolojia za Tehama za kisasa kama vile big data na akili bandia kuonesha vitu vyetu kwa umma, wenzetu na siku za zamani."

    Mwishoni mwa miaka ya 80 ya karne iliyopita, China ilianza shughuli za utafiti wa mambo ya kale chini ya maji. Na ushirikiano kati ya China na Kenya katika utafiti huo ulianza mwaka 2010.

    Anasema, "Watu wa jumba la makumbusho la taifa la China tuna haki ya kuzungumzia shughuli za akiolojia chini ya maji nchini China, kwani shughuli hizo zilianzishwa na jumba letu. Akiolojia majini na mashambani zinahimizana na kusaidiana. Kwa njia hii tutaweza kuelewa vizuri maana ya utamaduni wa kichina na mawasiliano kati utamaduni wetu na wa nchi za nje."

    Kuanzishwa kwa utafiti wa mambo ya kale chini ya maji ni matunda ya mageuzi na ufunguaji mlango wa China, na jumba la makumbusho la taifa la China nalo linaongeza ushirikiano na majumba mengine ya nchi zilizo katika "Ukanda Mmoja, Njia Moja". Bw. Wang amesema katika siku za baadaye, jumba la makumbusho la taifa la China litaitikia pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" kuongeza ushirikiano na nchi za Afrika, kuongeza maelewano kati ya watu na kuingiza uhai na mchango kwenye ushirikiano wa kitamaduni kati ya China na nchi za nje.

    Anasema, "Tunapendekeza kama kuna uwezekano wa kufanya onyesho la pamoja la majumba ya makumbusho ya nchi zilizo katika "Ukanda Mmoja, Njia Moja". Kila nchi inatoa vitu vinavyoweza kuwakilisha utamaduni wake, na kuoneshwa kwa pamoja ili watazamaji waweze kujionea utamu wa ustaarabu wa nchi tofauti. Tunatumai kufanya ushirikiano na majumba mengine katika shughuli za akiolojia na kujadiliana kuhusu ustaarabu wa binadamu katika siku za zamani na za sasa, ili tuelewe zaidi historia zetu za mawasiliano ya watu kuhusu ustaarabu wa binadamu."

    Rais Xi Jinping wa China aliwahi kusema ustaarabu unang'ara kutokana na mawasiliano. Mawasiliano na kufunzana kuhusu ustaarabu ni injini muhimu ya kuhimiza maendeleo ya ustaarabu wa binadamu na amani ya dunia. Bw. Wang anasema, "Wakati tunapofanya mawasiliano ya ustaarabu, si tu tunaona vitu vizuri vyenye thamani ya utamaduni na historia, bali pia tunaweza kuhisia roho na yaliyomo ya kitamaduni viliyo nayo vitu hivyo. Kila utamaduni unastahili kujifunza, kuigwa ili kuongeza nafasi zetu za kujiendeleza."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako