• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mjumbe wa China asisitiza kuheshimu haki halali ya China katika WTO

    (GMT+08:00) 2018-05-18 18:54:36

    Mjumbe wa kudumu wa China katika Shirika la Kimataifa la Biashara WTO Bw. Zhang Xiangchen leo ametoa makala kwenye gazeti la Uswisi akisisitiza kuwa, China, ikiwa ni nchi inayoendelea ina haki ya kutendewa kwa tofauti, ambayo ni haki halali inayotolewa na WTO.

    Wakati huo huo, China pia inapenda kutekeleza majukumu makubwa zaidi, ili kutimiza mafanikio na maendeleo ya pamoja kupitia ushirikiano.

    Bw. Zhang Xiangchen amesema, baada ya kufungua mlango na kufanya mageuzi kwa miaka 40, China imepata maendeleo makubwa, lakini bado inakabiliana na changamoto na matatizo mengi wakati inapotimiza mambo ya kisasa kwa pande zote. China kwa mujibu wa kiwango chake cha maendeleo na uwezo wake, imebeba wajibu mkubwa wa kufungua mlango kuliko nchi nyingine zinazoendelea hata nchi zilizoendelea. Pia China inapenda kushirikiana na nchi mbalimbali kujadili namna ya kuendelea kwa pamoja, na kutekeleza majukumu yake makubwa zaidi ili kutimiza ushirikiano wa kunufaishana na kuendelea kwa pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako