• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kodi yaongezwa kwa mafuta ghafi Tanzania

    (GMT+08:00) 2018-05-18 19:09:07

    Serikali ya Tanzania imesema itaongeza kodi kwenye mafuta ghafi yanayoingizwa nchini humo kutoka asilimia 10 hadi 25.

    Wizara ya Kilimo pia imewasilisha Wizara ya Fedha na Mipango mapendekezo ya kuboresha mfumo wa kodi na tozo kwa lengo la kuboresha mazingira ya uwekezaji na uendeshaji biashara kwenye shughuli za kilimo.

    Waziri wa Kilimo, Dk. Charles Tizeba amesema, kodi ya mafuta ghafi inaongezwa ili kuhamasisha uwekezaji katika mazao ya mafuta na kwamba, ongezeko hilo litatumika kuendeleza uzalishaji wa mbegu za mafuta.

    Amesema uzalishaji wa mazao ya mbegu za mafuta za alizeti, karanga, ufuta, mawese na soya umeongezeka kwa viwango tofauti.

    Amefafanua kuwa kuongezeka kwa uzalishaji kumechangiwa na kuongezeka kwa hamasa kwa wakulima kutokana na uwepo wa soko la uhakika, ushirikiano kati ya sekta ya umma na sekta binafsi pamoja na uwekezaji katika viwanda vidogo na vya kati vya kusindika mazao hayo katika mikoa ya Manyara, Singida, Dodoma, Mbeya, Katavi, Lindi, Mtwara, Iringa, Njombe, Rukwa na Kigoma.

    Amesema, inalenga kuhamasisha uzalishaji alizeti kutoka tani 3,112,500 mwaka 2016/2017 hadi tani 9,337,500 ifikapo mwaka 2021/2022 na kuongeza tija kutoka tani 1.5 hadi tani 3 kwa hekta.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako