v Watu waipongeza China kwa kupata maendeleo makubwa katika uchumi wa kidijitali
Ikiwa imetimia miaka 40 tangu China ianze kutekeleza sera ya mageuzi na ufunguaji mlango, mkutano wa kwanza wa kilele wa kujenga China ya kidijitali umefanyika huko Fuzhou, kusini mashariki mwa China. Washiriki wa mkutano huo wanaona mkutano huo utaifahamisha zaidi dunia kuhusu maendeleo iliyopata China katika sekta ya uchumi wa kidijitali katika miaka ya hivi karibuni, kuhimiza mawasiliano na mabadilishano ya uzoefu kati ya China na nchi za nje na kuimarisha zaidi ushirikiano.
|