• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Marekani zatoa taarifa ya pamoja kuhusu mkutano wa mashauriano ya kiuchumi na kibiashara

    (GMT+08:00) 2018-05-20 10:37:07
    China na Marekani jana zimetoa taarifa ya pamoja kuhusu mashauriano ya kiuchumi na kibiashara, zikiwekeana nadhiri ya kutoanzisha vita vya kibiashara dhidi ya zenyewe.

    Kwa kufuata mwongozo wa Rais Xi Jinping wa China na Rais wa Marekani Donald Trump, ujumbe kutoka China na Marekani ulifanya mashauriano thabiti kuhusu biashara siku za Alhamisi na Ijumaa.

    Pande zote mbili zilikubaliana kuchukua hatua zenye kufaa ili kuhakikisha zinapunguza mapungufu ya kibiashara kati China na Marekani.

    Kipekee China itaongeza manunuzi ya bidhaa na huduma kutoka Marekani ili kukidhi mahitaji ya watu wa China na kusukuma mbele maendeleo bora ya uchumi wake, jambo ambalo pia litasaidia maendeleo ya kiuchumi ya Marekani na kuongeza ajira.

    Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mataifa mawili hayo yamekubaliana kwa dhati kuongeza uuzaji na usafirishaji wa bidhaa za kilimo na nishati kutoka Marekani. Upande wa Marekani utatuma ujumbe wake nchini China kwa ajili ya mashauriano zaidi.

    Katika hatua nyingine, pande hizo mbili zilijadili kuhusu upanuzi wa biashara ya bidhaa zinazozalishwa viwawandani na huduma, na zimekubaliana kuunda mazingira rafiki ili kukuza biashara katika maeneo hayo.

    Taarifa hiyo imesema kwamba pande hizo mbili pia zilijadili kwa kina kuhusu ulinzi wa hakimiliki ya uvumbuzi na zikakubaliana kuongeza ushirikiano kwenye hilo.

    Pande hizo mbili zimekubaliana kuendeleza kufanya uwekezaji upande mmoja kwenda mwingine, na zikiweka nia ya kuweka mazingira ya kibiashara yenye usawa.

    Ujumbe wa China uliongozwa na mjumbe maalum wa Rais Xi ambaye pia ni naibu waziri mkuu Liu He, na kwa upande wa Marekani ilijumuisha waziri wa fedha wa nchi hiyo Steven Mnuchin, waziri wa biashara Wibur Ross na mwakilishi kutoka idara ya biashara Robert Lighthizer.

    Liu aliwasili mjini Washington siku ya Jumanne mchana kwa ajili ya mkutano wa mashauriano ya kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani ikiwa ni kwa mwaliko wa Marekani.

    Liu pia ni mjumbe wa kamati ya siasa ya kamati kuu ya Chama cha kikomunisti cha China CPC na ndiye aliyekuwa mkuu wa upande wa China kwenye mkutano huo wa majadiliano ya hali ya juu wa uchumi, akiongoza ujumbe ambao wajumbe wake wanatoka katika sekta kuu za kiuchumi za serikali ya China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako