• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Marekani zakubaliana kutofanya vita vya kibiashara

    (GMT+08:00) 2018-05-20 10:37:46
    Mwakilishi wa rais Xi Jinping ambaye ni naibu waziri mkuu wa China, Bw Liu He amesema, China na Marekani zimefikia makubaliano kuhusu masuala ya kichumi na kibiashara, zikiahidiana kutoanzisha vita vya kibiashara na kusimamisha hatua za kuongeza kutoza ushuru wa forodha dhidi ya bidhaa za pande mbili.

    Liu ameyasema hayo kabla ya kurudi nyumbani, baada ya ujumbe ulioongozwa naye kuwa na mkutano wa mashauriano na ujumbe wa Marekani siku za Alhamisi na Ijumaa.

    China na Marekani zitaongeza ushirikiano wa kibiashara katika fani za nishati, bidhaa za kilimo, afya, bidhaa za teknolojia za hali ya juu na mambo ya kifedha. Bw Liu He alisema, hatua hizo zitanufaisha pande mbili, kwa kuwa zitachangia juhudi za China za kuinua kiwango cha maendeleo ya uchumi wa China na kulingana na mahitaji ya watu wake, pia kuisaidia Marekani inayojitahidi kupunguza nakisi ya kibiashara.

    Hata hivyo Liu alisisitiza kuwa, China yenye idadi kubwa ya watu wa mapato ya wastani itabadilika kuwa soko kubwa zaidi duniani. Na hilo ni soko lenye ushindani mkali, ambapo nchi nyingine zinapaswa kujiimarisha ziwe na nguvu ya ushindani ya bidhaa na huduma zake ili kupata mgao mkubwa zaidi kwenye soko la China na kuvutia watu wa China. Bw Liu aliongeza kuwa, si kama tu China inapenda kufanya manunuzi kutoka Marekani, bali pia kutoka nchi nyingine duniani.

    Akijumuisha mazungumzo yaliyomalizika, Liu alisema inahitaji muda katika kutafuta utatuzi wa masuala ya kimuundo kati ya China na Marekani ambayo yamekuwepo kwa miaka mingi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako