• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China Xi Jinping na mkewe Peng Liyuan

    (GMT+08:00) 2018-05-20 15:22:37

     

    Leo tarehe 20 Mei imebadilika kuwa sikukuu mpya nchini China, kwani matamshi ya "Mei 20" kwa lugha ya Kichina yanafanana na neno "Nakupenda". Leo hii watu wanapotaja mapenzi, wanamzungumzia sana rais wa China Xi Jinping na mkewe Peng Liyuan.

    Xi Jinping anathamini sana familia, wazazi, mke na mtoto ambao ni watu muhimu sana kwake. Yeye na mkewe Peng Liyuan, wanapendana na kusaidiana, wakisifiwa na watu wa China kuwa mume na mke wa mfano.

    Xi Jinping na Peng Liyuan walifunga ndoa mwezi Septemba mwaka 1987. Hawakuandaa sherehe kubwa ya harusi, bali marafiki na wafanyakazi wenzao walialikwa kula chakula kwa pamoja. Mapenzi ni kumilikiana na mapenzi ya kweli huleta furaha moyoni.

    Baada ya harusi, Xi Jinping alisafiri kikazi mara kwa mara, Peng Liyuan ambaye ni mwimbaji wa jeshi, pia alipaswa kutembelea makambi ya kijeshi kote nchini China kufanya maonyesho. Hata hivyo walielewana na kufuatiliana. Xi Jinping alipofanya kazi mkoani Fujian ambapo hali ya hewa ni baridi, mkewe alimtengenezea blanketi, huku Peng Liyuan alipofanya maonyesho mkesha wa mwaka mpya, mumewe alipika chakula akimsubiri arudi na kula kwa pamoja. Walimpatia binti yao jina la Mingze, maana yake ni kuwa mtu msafi.

    Xi Jinping anayethamini sana familia, anachukulia kazi ya kufanikisha furaha ya familia za wananchi ni kazi yake ya kimaisha. Anasema "Hatuwezi kulegeza hata kidogo mpaka tutimize ndoto ya wananchi ya kuishi kwa furaha. Ni lazima tukiongoza wananchi tuchape kazi kwa pamoja."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako