• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakati umefika wa China na Marekani kutafsiri maana halisi ya kunufaishana katika uchumi na biashara

    (GMT+08:00) 2018-05-20 16:17:49

    China na Marekani jana zimefanya kikao kizito na kigumu cha mashauriano, kilichomalizika kwa makubaliano ya kutoanzisha na kushiriki vita vya kibiashara.

    Katika taarifa ya pamoja iliyotolewa siku hiyo hiyo, mataifa mawili hayo yaliwekeana nadhiri ya kuimarisha ushirikiano wao wa uchumi na kibiashara.

    Awamu hii ya ujumbe wa China nchini Marekani imekuwa na matokeo chanya, utekelezaji kwa vitendo, yenye kujenga na kuleta maendeleo. Kwani imefanikisha utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa awali na wakuu wa nchi hizo mbili na imesaidia kuwatia moyo watu wa nchi hizo mbili na jumuiya ya kimataifa.

    Kuanzia ziara ya Washington ya mwezi Februari ya kiongozi mwandamizi wa China Bw. Liu, hadi ziara ya ujumbe wa Marekani nchini China mwezi Mei, mawasiliano kwa njia ya simu ya hivi karibuni kati ya Rais wa China Xi Jinping na mwezake wa Marekani, Donald Trump, na ziara ya hivi karibuni ya mjumbe wa Rais Xi, matokeo ya mwisho ni kwamba majibizano haya yamethibitisha ujumbe kuwa, nchi hizi mbili zenye uchumi mkubwa duniani zinafanya juhudi ya kuondoa tofauti kati ya zenyewe chini ya mwongozo wa maafikiano yaliyofikiwa na marais wan chi hizo mbili.

    Mataifa hayo kwa sasa yameingia makubaliano kwenye maeneo mengi, mfano nishati, bidhaa za kilimo, afya, teknolijia ya hali ya juu na Fedha. Vile vile zimekubaliana kuimarisha ushirikiano kwenye kulinda haki miliki ya uvumbuzi kwenye uwekezaji kwa pande zote mbili.

    Matokeo chanya hayo yasingewezekana bila ya maafikiano kati ya Xi na Trump, na ahadi zilizowekwa katika ushirikiano wan chi hizo mbili ili kuondoa tofauti za kiuchumi na biashara zilizojitokeza.

    Kutokana na kutofautiana kwa pande mbili katika maeneo kama muundo uchumi na utambuzi wa utamaduni, maafikiano kwenye tofauti za kibiashara yasingewezekana na yangehitaji ahadi za utekelezaji wa muda mrefu.

    Kwa hiyo, huu ni mwanzo mzuri wa kuona matokeo ya mashauriano ya sasa, hasa baada ya nchi mbili hizi zilizokuwa zinavutana. Na kwa kufuata kanuni ya kuheshimiana na ushirikiano wa kunufaishana, China na Marekani zitaweza kuondo vikwazo pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako