• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Washiriki wa Mkutano wa Baraza la China na utandawazi wa dunia wasifu mafankio ya taarifa ya pamoja kati ya China na Marekani

    (GMT+08:00) 2018-05-20 20:33:46

    China na Marekani jana huko Washington zimetoa taarifa ya pamoja kuhusu mkutano wa mashauriano ya kiuchumi na kibiashara kati yao. Kwenye mkutano wa nne wa Baraza la China na utandawazi wa dunia uliofanyika leo hapa Beijing, washiriki wengi wamekaribisha taarifa hiyo. Wameona kuwa, kuzidisha ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani si kama tu kunaweza kukidhi mahitaji ya wananchi wa nchi hizo mbili, bali pia kunaamtana na mahitaji ya utandawazi wa dunia.

    Naibu mkurugenzi wa mradi wa utafiti wa China wa Freeman Chair Bw. Scott Kennedy amesema China na Marekani zimefikia maoni ya kutofanya vita vya kibiashara, hii ni vizuri sana.

    Mkuu wa zamani wa kampuni ya Sinopec Bw. Fu Chengyu amesema, taarifa ya pamoja kati ya China na Marekani inaonesha mabadiliko ya uhusiano wa uzalishaji duniani. Amesema,

    "Maoni sita ya pamoja kwenye taarifa ya pamoja ni matokeo ya ushirikiano wa kupata maendeleo ya pamoja. Uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani, si kama tu ni biashara yenyewe, bali pia ni matokeo ya lazima katika mchakato wa mabadiliko ya uhusiano wa dunia au mabadiliko ya uhusiano wa uzalishaji."

    Katibu mkuu wa zamani wa Baraza la Asia la Bo'ao Bw. Long Yongtu amesema,

    "China na Marekani zimefikia maoni ya pamoja, kutokana na matumaini ya kisiasa ya viongozi wa nchi hizo mbili. Vilevile hii ni mahitaji ya wananchi wa nchi hizo mbili. Utandawazi wa dunia umeunganisha maslahi ya nchi hizo mbili na wananchi wao, tumechagua njia ya kunufaishana na kupata maendeleo ya pmoja. "

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako