China imerusha satelaiti inayounganisha mawasiliano kati ya dunia na chombo cha kuchunguza sayari ya mwezi cha Chang'e No. 4, ambacho kitachunguza upande wa mbali wa sayari hiyo ulioko kizani. Satelaiti hiyo iitwayo Queqiao, imerushwa mapema leo kwa kutumia roketi aina ya Long March-4C kutoka kwenye kituo cha kurushia satelaiti cha Xichang, kusini magharibi mwa China.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |