• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kusaidia utafiti na maendeleo ya teknolojia ya VR

    (GMT+08:00) 2018-05-21 18:09:58

    China inatarajiwa kutunga sera kwa ajili ya kusaidia utafiti na maendeleo ya teknolojia ya uvumbuzi wa hali ya bandia inayoendana na hali halisi VR, na kuiunganisha na sekta zingine.

    Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari, naibu waziri wa Viwanda na Mawasiliano Luo Wen amesema wizara hiyo itaharakisha uanzishwaji na ufanyaji wa mabadiliko ya ubora wa viwanda kwa kuwezesha matumizi ya teknolojia ya VR na matokeo yake katika maeneo mengine.

    Teknolojia ya VR imeonekana ikiendelea kwa kasi nchini China. Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Wizara ya Viwanda na Mawasiliano, Soko la VR lilikua na kufikia asilimia 164 hadi mwaka 2017 sawa na dola za kimarekani bilioni 2.5.

    VR ni teknolojia ya matumizi ya kompyuta kuonyesha mazingira bandia kwa muonekano hali ya ung'aavu unaoakisi mazingira halisi, ambapo kwa kutumia baadhi ya vifaa kama kofia ngumu na miwani watumiaji huhisi kama wapo katika mazingira halisi wawapo kwenye mazingira hayo bandia.

    VR inaweza kutumika kutengeneza akili bandia, pia inaweza kutumika kwenye elimu na mafunzo, sekta ya afya, michezo, utalii na jamii za kufikirika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako