• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuendelea kufanya juhudi ili kulinda na kutekeleza makubaliano ya pande zote ya suala la nyuklia la Iran

    (GMT+08:00) 2018-05-21 18:51:50

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Lu Kang amethibitisha kuwa China itashiriki mkutano wa kamati ya pamoja ya makubaliano ya pande zote ya suala la nyuklia la Iran, huku akisisitiza kuwa China itaendelea kufanya juhudi ili kulinda na kutekeleza makubaliano hayo.

    Mei 25, Iran, China, Russia, Ufaransa, Ujerumani na Uingereza zitafanya mkutano wa kamati ya pamoja ya makubaliano ya pande zote ya suala la nyuklia la Iran. Naibu waziri wa mambo ya nje wa Iran Bw. Abbas Araqchi amesema, mkutano huo utajadili kuhusu athari zinazoletwa na kujitoa kwa Marekani kutoka makubaliano hayo na jinsi pande zinazosalia zinavyoendelea kutekeleza makubaliano hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako