• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: kaunti 14 bado hazija tumia fedha zozote katika miradi ya maendeleo

    (GMT+08:00) 2018-05-21 19:04:26

    Katika kipindi cha miezi 6 hadi Desemba, kaunti 14 bado hazija tumia fedha zozote katika kufanya miradi yeyote ya maendeleo, jambo ambalo limeathiri nafasi za kazi na miradi ya miundombinu katika vitengo vilivyotengwa.

    Mdhibiti wa Bajeti Agnes Odhiambo, katika ripoti ya nusu ya mwaka wa mwaka 2017/18, alitaja Embu, Garissa, Kirinyaga, Kisumu, Meru, Nakuru, Nandi, Nyandarua na Nyeri kama kaunti zilizoathiriwa.

    Matumizi ya maendeleo ni muhimu kujenga miundombinu kama barabara na maji taka na kuweka pesa kwa mikono binafsi kupitia mahitaji ya malighafi, ambayo hatimaye inajenga nafasi za ajira mpya.

    Katika muda wa miezi sita, kaunti zilitumia Sh bilioni 11.4 katika miradi ya maendeleo, kutoka Sh bilioni 35.7 iliyotumiwa wakati sawa huu, mwaka uliopita.

    Ripoti pia imetia wasiwasi juu ya kupungua kwa mapato yaliyokusanywa na kaunti, mapato ya kila mwaka ya paswa angalau kufika Sh bilioni 55.

    Lakini kaunti zimeweza kukusanya Sh bilioni 9.9 ambayo ni asilimia 18.1 ya lengo la kila mwaka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako