• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: benki ya kcb, na equity imetangaza faida ya dola milioni 108.25

    (GMT+08:00) 2018-05-21 19:04:48

    benki mbili nchini Kenya zimetangaza faida ya pamoja ya dola milioni 108.25 katika miezi mitatu ya kwanza ya mwaka huu, na kupuuza matarajio ya chini ya kipindi hicho licha ya kuongezeka kwa mikopo isiyo na manufaa.

    Benki za Equity zilitangaza kupanda kwa asilimia 21.7 kwa faida yake baada ya kodi na kufikia dola milioni 58.24 kwa miezi mitatu iliyoisha Machi, na kushinda benki ya KCB ambaye ameandikisha $ milioni 50.25 kwa kipindi kama hicho.

    Kitabu cha mikopo cha Equity kiliongezeka kwa dola milioni 90.53 hadi dola bilioni 2.68 katika miezi mitatu, ambayo iliona jumula ya riba ilipanda kwa asilimia 10.5 na kufikia dola milioni 124.4.

    Mapato ya riba, kutoka kwa mikopo na maendeleo iliongezeka kwa asilimia 6.97 na kufikia dola milioni 86.49.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako