• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania:china ya patia tanzania fedha ya msaada sh146bn kupiga jeki miundombinu.

    (GMT+08:00) 2018-05-21 19:05:27

    Tanzania imepokea msaada wa kifedha sh bilioni 146 .47 kutoka kwa serikali ya China kwa ajili ya miradi miwili mikubwa ya miundombinu.

    Katibu wa kudumu wa Fedha na Mipango Dotto James ndiye aliyetia saini kwa niaba ya serikali ya Tanzania wakati balozi wa China nchini Tanzania Wang Ke aliyesaini kwa niaba ya nchi yake.

    Bwana James alifafanua kuwa fedha hizo zilikuwa ni msaada na si mkopo na zitatumika kwenye miradi miwili ya miundombinu, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa chuo kikuu cha usafirishaji wa kitaifa kwa gharama ya dola milioni 62 sawa na Sh bilioni 138.3.

    Katika mradi wa pili, jumla ya Sh bilioni 3.2 itatumika kwenye utafiti wa upembuzi wa mradi mpya wa Standard Gauge Rail (SGR).

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako