• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kesi ya Viongozi wa Soka Tanzania, Mtendaji mkuu wa ligi aenda kutoa ushihidi mahakamani

  (GMT+08:00) 2018-05-22 08:33:39

  Nchini Tanzania, mtendaji mkuu wa bodi ya ligi za soka Boniface Wambura jana alifika mahakamani mjini Dar es Salaam kutoa ushahidi kwenye kesi inayomkabili rais wa zamani wa shirikisho la mpira wa miguu TFF, Jamal Malinzi na wenzake wanne.

  Mahakamani hapo, shahidi huyo aliukana na kudai kuwa ni wa kugushi muhtasari wa kikao ambao unaonyesha yeye ni mmoja wa washiriki, jambo ambalo alilipinga.

  Kikao hicho ndicho kinachodaiwa kubadilisha watia saini katika akaunti za benki za TFF, jambo linalodaiwa kuwa lilifungua milango ya ufujaji na ubadhilifu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako