• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China inapenda kushirikiana na nchi nyingine kupunguza kukosekana kwa haki kwenye huduma za afya

    (GMT+08:00) 2018-05-22 09:52:47

    China inapenda kushirikiana na nchi nyingine ili kupunguza tatizo la kukosekana kwa haki kwenye masuala ya afya na kutoa huduma bora za afya kwa wote.

    Hayo yamesemwa na mkurugenzi wa Tume ya Afya ya Taifa ya China Bw. Ma Xiaowei kwenye kikao cha 71 wa Baraza Kuu la Afya Duniani kilichofunguliwa jana mjini Geneva. Amesema China inatilia maanani umuhimu wa kuanzisha mfumo wa huduma za afya na matibabu zenye ubora na ufanisi na kufanya kila iwezalo kuwawezesha watu kumudu huduma hizo.

    Ameongeza kuwa China inajitahidi kushiriki kwenye usimamizi wa masuala ya afya duniani na kuhimiza ujenzi wa jumuiya yenye hatma ya pamoja na kusaidia nchi zinazoendelea kutimiza malengo yao ya kiafya.

    Kikao cha 71 cha mwaka cha Baraza Kuu la Afya Duniani kimehudhuriwa na wajumbe karibu elfu nne kutoka nchi wanachama 194 wa Shirika la Afya Duniani WHO na mashirika wenza. Baraza Kuu la Afya Duniani ni bodi ya juu zaidi ya WHO inayofanya maamuzi, kutunga sera na kuidhinisha bajeti ya Shirika hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako