• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Waelekezi matapeli waathiri sekta ya utalii Uganda

    (GMT+08:00) 2018-05-22 21:11:02

    Tatizo la waelekezi matapeli wa watalii linaonekana kukita mizizi kwenye sekta ya utaii nchini Uganda. Inasemekana kwamba waelekzi hawa ambao wamekuwa wakijitajirisha kwa utapeli, huwa wanawakodeshea watalii hoteli ambazo hazifai au hata kuwapa vibali bandia vya kuzuru mbuga mbali mbali za wanyamapori. Kwa sasa, sekta ya utalii Uganda inachangia asilimia 10 ya mapato ya taifa. Utalii unaingiza takribani dola bilioni 1.4 kila mwaka. Inatarajiwa kuwa ifikapo mwaka wa 2020, sekta ya utalii itakuwa ikiingiza takribani dola bilioni 2.4. Hivyo basi, ili hili liafikiwe, lazima swala la waelekezi matapelki kushughulikiwa haraka iwezekanavyo. Shirika la usafiri wa watalii la Uganda Safaris and Guides Association limeaomba serikali kuu ya Uganda kuingilia kati na kuziba mianya iliyopo kwenye sekta ya utalii, haswa utapeli.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako