• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya: Wauzaji makaa wataka marufuku ya ukataji miti kuondolewa.

  (GMT+08:00) 2018-05-22 21:11:41

  Baada ya kuonekana kwamba mazingira yanaathiriwa sana kutokana na ukataji wa miti, serikali ya Kenya ilipiga marufuku ukataji wa miti kiholela na tena bila idhini. Mojawapo ya maeneo yalioathirika sana na marufuku haya ni wakazi wa eneo la Mwatate, katika kaunti ya Taita Taveta.

  Wakazi hao sasa wanasema kwamba wamesalia bila ajira kwa sababu hawauzi tena makaa kama ilivyokuwa hapo awali, ili kukimu mahitaji yao. Wafanyibiashara hao wameongeza kwa kusema kuwa endapo serikali haitafutilia mbali marufuku ya uchomaji wa makaa, basi wengi wao watazidi kuzama kwenye lindi la ulevi na uraibu wa pombe na mihadarati.

  Vijana wengi ambao walikuwa wakitegeme sana biashara ya makaa, wanasema kwamba amri aliyoitoa naibu Rais William Ruto ya kutokata miti alipozuru eneo hilo, imewaacha vijana wengi wakilala hoi, maskini hohe hahe. Wametaja ongezeko la makundi ya uhalifu kutokana na ukosefu wa ajira. Kilio chao ni kwamba, serikali kuu itupilie mbali marufuku haya, ili warejelee kazi yao ya uuzaji makaa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako