• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya: Wakuzaji nafaka wataka kaunti zisimamie Bodi ya Kitaifa na Nafaka na Mazao.

  (GMT+08:00) 2018-05-22 21:12:03

  Wakulima wa nafaka kutoka eneo la Kaskazini mwa Bonde la Ufa, wameomba serikali kuu kukabidhi usimamizi wa Bodi ya Nafaka na Mazao nchini Kenya yaani NCPB kwa serikali za kaunti.

  Wakulima waliafikia uamuzi huu kwa kusema katiba imesema wazi kuwa jukumu la kusimamia kilimo ni la serikali za kaunti, na hii itraboresha usimamizi wa bodi hiyo kwa kuhakikisha kuwa wakulima wanalipwa pesa zao kwa wakati ufaao na pembejeo kusambazwa vyema. Vile vile, wakulima hao waliongeza kwa kusema kuwa magavana na maafisa wa kilimo kwenye kaunti, wanaelewa fika changamoto zinazowakumba wakulima katika maeneo yao, hivyo basi wapewe jukumu kubwa la kusimamia Bodi ya Nafaka na MAzao nchini Kenya NCPB.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako