• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • WHO yasema dunia iko njia panda katika kutokomeza malaria

  (GMT+08:00) 2018-05-23 09:17:24

  Kwenye mkutano wa shirika la afya duniani WHO unaoendelea mjini Geneva, imefahamika kuwa kwa sasa dunia iko njia panda kwenye vita dhidi ya ugonjwa wa malaria.

  Naibu mkurugenzi wa WHO Bw. Ren Minghui amesema kama dunia haitabadilisha mambo kwa sasa, itakuwa vigumu kutokomeza ugonjwa wa malaria katika nchi nyingine 10 kabla ya mwaka 2020, au kupunguza asilimia 90 ya vifo kabla ya mwaka 2030.

  Naibu waziri wa kamati ya afya ya taifa Bw. Cui Li amesema China inakaribia kufanikiwa kutokomeza ugonjwa huo, kutoka mtu mmoja kuambukizwa kati ya watu elfu 10 katika mwaka 2010, na kuwa maambukizi sifuri mwaka 2017. 

  Changamoto kubwa ya ugonjwa wa malaria bado iko barani Afrika, ambako asilimia 90 ya maambukizi yote milioni 200 duniani kwa mwaka yako barani huo.

  Nchi za Asia Kusini Mashariki, zimesaini mpango wa utekelezaji na China, unaoitwa "Kanda Moja, Mkakati mmoja" ili kuwa mwongozo wa kutokomeza ugonjwa wa malaria kwenye kanda hiyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako