Takwimu zilizotolewa na mamlaka za Somaliland zinaonyesha kuwa, watu 12 wakiwemo watoto wamejeruhiwa katika maafa hayo. Taarifa iliyotolewa na ofisi ya rais pia inasema familia laki 1.6 zilizopo kwenye eneo la pwani zimeathiriwa na kimbunga hicho.
Shirika la hisani la kimataifa Save the Chidren limeonya kuwa hali ya maisha ya watoto itakuwa mbaya zaidi kutokana na ukosefu mkubwa wa chakula, kupoteza makazi na magonjwa yanayoweza kuenea kwa maji baada ya maafa hayo kutokea.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |