• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Makampuni ya China na Kenya yaahidi kuongeza ushirikiano

  (GMT+08:00) 2018-05-23 10:07:15

  Makampuni ya China yameahidi kushirikiana na wenzao wa Kenya kusaidia maendeleo ya uchumi na jamii chini ya pendekezo la "Ukanda Mmoja,Njia Moja" na kuisaidia nchi hiyo kutimiza ajenda yake ya maendeleo ya BigFour uliowekwa na rais Uhuru Kenyatta.

  Ahadi hiyo imetolewa kwenye kongamano la kwanza la makampuni ya China na Kenya lilioandaliwa na Chama cha wafanyabiashara wa China na Kenya na makundi mengine ya Kenya.

  Konsela wa uchumi na biashara wa ubalozi wa China nchini Kenya Bw. Guo Ce, amesema kuongeza ushirikiano kati ya makampuni ya China na Kenya ni muhimu katika kuleta maslahi ya pamoja kwao.

  Bw. Guo amesema serikali ya China na makampuni ya China wamekuwa wakiunga mkono nia ya Kenya kutimiza ajenda yake ya maendeleo ya BigFour ikiwa ni pamoja na usalama wa chakula, uzalishaji viwandani, nyumba za bei nafuu na huduma za afya wa wote.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako