• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yafanya msako wa kuingiza taka kimagendo, tani 137,000 zakamatwa

    (GMT+08:00) 2018-05-23 16:45:37

    Mamlaka ya forodha nchini China imekamata tani laki 1.37 za taka haramu zilizoingizwa nchini katika kile kinachoitwa kampeni kubwa zaidi dhidi ya uingizaji haramu wa taka katika miaka ya karibuni.

    Taarifa iliyotolewa na Ofisi Kuu ya Usimamizi wa Forodha ya China (GAC) imesema, taka hizo ni pamoja na vyuma chakavu na mabaki ya madini, na kuongeza kuwa pia imepata ushahidi wa tani 606, 500 za taka ngumu zilizoingizwa nchini, ikiwemo taka za plastiki.

    China ilianza kuagiza taka ngumu kama chanzo cha mali ghafi katika miaka ya 1980, na kwa miaka kadhaa imekuwa nchi inayoongoza duniani kwa kuagiza taka ngumu, licha ya uwezo wake mdogo wa kuangamiza takataka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako