• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania-Wafugaji wakwepa ushuru

    (GMT+08:00) 2018-05-23 20:03:19

    Wafugaji katika wilaya ya Longido mkoani Arusha wanaouza mifugo yao nchini Kenya wamelalamika kutozwa Sh20,000 kwa ng'ombe mmoja wakidai kuwa kiasi hicho ni kikubwa.

    Kutokana na tatizo hilo,wafugaji hao wamedai kwamba baadhi yao wanalazimika kukwepa kutumia mnbada wa mifugo na badala yake wanatumia njia za panya.

    Kaimu Ofisa Mifugo wilayani Longido,Nestory Dagharo,alisema hayo alipokuwa akiwasilisha taarifa za maendeleo ya mnada wa mifugo kwa kamati ya siasa ya wilaya.

    Alisema ili kukabiliana na changamoto ya wafanyabiashara kutumia njia za panya kusafirisha mifugo ,wanalazimika kufanya doria mchana na usiku ili kudhibiti.

    Alisema kuna umuhimu wa wafanyabiashara kupewa elimu juu ya mwingiliano wa kibiashara baina ya nchi mbili tofauti kutokana na baadhi yao kutokuwa na uelewa na utaratibu wa uendeshaji wa biashara zao nje ya nchi.

    Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Longido,Godfrey Chongolo,alisema mnada huo ni mali ya halmashauri ya wilaya hiyo,hivyo anategemea ajira nyingi zitawalenga wakazi husika wa eneo hilo pamoja na kufanya operesheni kwa wanaovusha mifugo kwa kutumia njia zisizo sahihi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako