• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya-Bei ya mchele yashuka kwa asilimia 21 kutokana na kuongezeka kwa uzalishaji

    (GMT+08:00) 2018-05-23 20:04:06

    Bei ya mchele katika mpango wa umwagiliaji wa Mwea nchini Kenya imeshuka kwa asilimia 21 kutokana na kuongezeka kwa uzalishaji.

    Bei ya kilo moja ya bidhaa hiyo imeshuka kutoka Sh 170 mwezi Mei mwaka jana hadi Sh140.

    Hata hivyo uzalishaji umeongezeka mara tatu kutoka tani 25,369 katika msimu wa mwaka 2016/2017 hadi tani 75,094 katika msimu wa mwaka 2017/2018 .

    Uzalishaji wa mchele katika msimu uliopita uliathiriwa kwa kiasi kikubwa na ukame na umwagiliaji mkubwa katika mto Thilba ambao unahudumia asilimia 80 ya eneo la umwagiliaji la Mwea.

    Uhaba wa mchele nchini Kenya mwaka jana ulisababisha bidhaa hiyo kuuzwa hadi Sh.200 kwa kilo.

    Bei hiyo ilikuwa juu zaidi kwa wauzaji rejareja ambao waliuza mchele hadi shilingi 250.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako