• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania-Baraza la TCRA-TCC lazitaka Kampuni za Simu kuhakikisha usalama wa watumiaji wa mitandao hiyo dhidi ya utapeli

    (GMT+08:00) 2018-05-23 20:05:30

    Baraza la ushauri la watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Tanzania (TCRA-CCC),limezitaka kampuni za simu kutimiza wajibu wao wa kisheria kwa kuhakikisha usalama wa watumiaji wa mitandao hiyo dhidi ya wahalifu.

    Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na wahalifu wa mitandao ambao wanatumia simu za mikonono kutuma jumbe mbalimbali za kuomba fedha na utapeli jambo linalosababisha usumbufu kwa watumiaji wa huduma hizo.

    Akizungumza jana jijini Dar es Salaam,Katibu Mtendaji wa TCRA-CCC,Mary Msuya,alisema kumekuwa na malalamiko yanayotolewa na watumiaji wa mitandao wanaopokea kupitia simu za mikononi na kwenye mikutano.

    Alisema matukio hayo yamekuwa na wahalifu wanaomiliki namba za simu zilizosajiliwa na kampuni za mitandao mbalimbali.

    Alisema katika kipindi cha miezi mitano kuanzia Januari mwaka huu,wamepokea simu za watumiaji wa mitandao 103 wakilalamikia kupokea ujumbe wa kitapeli.

    Pia alisema matukio hayo yameshamiri katika kipindi cha kuanzia mwaka huu na kwamba mtandao wa simu za mkononi wa Vodacom namba zake huwa zinatumiwa zaidi ya mitandao mingine.

    Aidha alisema wanachofanya kama TCRA-CCC,ni kutoa elimu na ushauri kwa watumiaji wa mitandao kabla ya kukumbwa na uhalifu huo na ikitokea mtumiaji ametapeliwa suala hilo wanaliachia jeshi la polisi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako