• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Pande hasimu Sudan Kusini zakamilisha mazungumzo ya amani

    (GMT+08:00) 2018-05-24 10:15:20

    Pande zinazopambana nchini Sudan Kusini zimekamilisha mazungumzo ya amani yaliyofanyika katika siku 6 zilizopita mjini Addis Ababa, Ethiopia, kwa lengo la kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.

    Pande zilizoshiriki kwenye mazungumzo hayo zimetangaza kuundwa kwa kamati ya uongozi na kamati ndogo ya usalama na usimamizi.

    Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Maendeleo ya Kiserikali ya nchi za Afrika Mashariki IGAD na waziri wa mambo ya nje wa Ethiopia Bw. Workneh Gebeyehu, amesema mazungumzo hayo ni uzoefu muhimu unaoweza kuisaidia IGAD kujifunza kutoka kwa "mawasiliano" kati ya pande hizo hasimu.

    Hata hivyo, Bw. Gebeyehu amesema licha ya mfululizo wa mazungumzo, maendeleo makubwa bado hayajapatikana.

    Mazungumzo hayo ya amani ya duru mpya yaliyofanyika chini ya upatanishi wa Baraza la Makanisa nchini Sudan Kusini SSCC, yalimalizika na mwito uliotolewa na IGAD wa kufanya kikao maalumu kujadili hatua za adhabu zitakazochukuliwa dhidi ya pande zitakazovunja makubaliano ya kusimamisha uhasama.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako