• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zambia yatoa mwito wa kutoa msaada wa fedha kwa wakimbizi wa DRC

    (GMT+08:00) 2018-05-24 10:16:00

    Serikali ya Zambia imezindua Mpango wa Kuwashughulikia Wakimbizi na kutoa mwito wa kuongeza msaada wa kifedha kwa wakimbizi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC waliopokelewa na nchi hiyo.

    Waziri wa Mambo ya Ndani wa Zambia Bw. Stephen Kampyongo amesema serikali ya nchi hiyo na washirika wake wanahitaji dola za kimarekani milioni 74.2 ili kuwahudumia ipasavyo wakimbizi wa DRC mwaka huu, lakini mpaka sasa ni dola za kimarekani milioni 8.3 tu zilizopatikana.

    Bw. Stephen ameongeza kuwa mahitaji ya misaada ya kibinadamu yanaweza kuongezeka kabla ya mwisho wa mwaka huu, wakati idadi ya wakimbizi wapya inatarajiwa kuongezeka kama hali ya DRC haibadiliki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako