• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wa Rwanda na Ethiopia kutembelea eneo la viwanda la Ethiopia lililojengwa na China

    (GMT+08:00) 2018-05-24 10:23:51

    Serikali ya Ethiopia imesema waziri mkuu wa Ethiopia Bw Abiy Ahmed na rais Paul Kagame wa Rwanda kesho watatembelea Eneo la viwanda la Hawassa nchini Ethiopia.

    Idara ya mawasiliano ya serikali ya Ethiopia imetoa taarifa ikisema katika ziara ya rais Kagame ya siku tatu nchini Ethiopia, rais huyo atatembelea eneo hilo la viwanda lililojengwa na China, na kujifunza uzoefu wa Ethiopia kwenye sekta za viwanda na miundombinu.

    Eneo hilo la viwanda lililojengwa na China kwa muda wa miezi tisa linatazamiwa na serikali ya Ethiopia kuwa mfano mzuri wa ujenzi wa maeneo ya viwanda nchini kote. Eneo hilo limepata mafanikio makubwa tangu lilipozinduliwa mwezi Juni mwaka 2016, na limevutia viwanda vingi vya vitambaa na nguo duniani.

    Zaidi ya hayo, eneo hilo linatarajiwa kuiletea Ethiopia mapato ya takriban dola bilioni moja za Marekani kwa mwaka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako