• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Ghana aamuru mwenyekiti wa shirikisho la soka akamatwe kutokana na kutapeli kwa kutumia jina la rais

    (GMT+08:00) 2018-05-24 10:41:55
    Rais Akufo-Addo wa Ghana ameamuru kukamatwa mwenyekiti wa shirikisho la Soka la Ghana Kwesi Nyantekyi, ambaye pia ni makamu mwenyekiti wa shirikisho la soka barani Afrika CAF, kufuatia makala moja ya uchunguzi kumhusisha na vitendo vya ulaghai. Inadaiwa Kwasi Nyantekyi alitumia jina la rais wakati akipanga na kutekeleza ulaghai wake. Uchunguzi huo ambao pia una ushahidi wa video, unadaiwa kufichua vitendo vya ufisadi miongoni mwa maofisa wengine wa shirikisho la soka la Ghana. Video hiyo inapangwa kuonyeswa kwa umma tarehe sita mwezi ujao. Lakini Kwesi Nyantenkyi aliyechaguliwa kuwa mwenyekiti wa shirikisho la soka nchini Ghana tangu mwaka 2005 na hajatamka lolote.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako