• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kocha wa zamani wa PSG Unai Emery ametangazwa kuwa kocha mpya wa Arsenal

  (GMT+08:00) 2018-05-24 10:48:35

  Mmiliki wa klabu ya Arsenal amemtangaza Emery mwenye miaka 46 kuwa kocha mpya wa klabu ya Arsenal, baada ya aliyekuwa kocha wa klabu hiyo Arsene Wenger kuagana na klabu hiyo. Emery amejiunga na Gunners akitokea PSG ambako aliwaongoza kushinda ligi kuu ya Ufaransa, Ligue 1. Kabla ya kujinga na Arsenal kulikuwa na habari kuwa kocha msaidizi wa Manchester City ambaye pia ni nahodha wa zamani wa Arsenal Mikel Arteta alipigiwa upatu sana kumrithi Wenger, lakini bahati haikuwa yake.

  Kwingineno mdudu wa timua timua na hamahama anaendelea kuonekana baada ya timu karibu zote za ulaya kumalizi misimu ya ligi.

  Kocha wa zamani wa Chelsea na Real Madrid Carlo Ancelotti ametangazwa kuwa kocha mpya wa klabu ya Napoli, akichukia nafasi ya Maurizio Sarri anayeachana na klabu hiyo. Sarri ametangazwa kuwa mrithi wa Antonio Comte ambaye mkataba wake na Chelsea umefika mwisho.

  Kocha wa zamani wa Man City Manuleo Pellegerini kutoka Chile, alisafiri kutoka hapa China baada ya kuacha kazi yake huko Hebei, kwenda kukamilisha taratibu za kuchukua mikoba ya David Moyes anayeagana na klabu ya Wesham baada ya mkataba wake kwisha.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako