• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waandishi wa habari wa Korea Kusini kukusanya taarifa za kufungwa kwa uwanja wa kufanyia majaribio ya nyuklia Korea Kaskazini

    (GMT+08:00) 2018-05-24 17:01:40

    Ujumbe unaoundwa na waandishi wanane wa habari wa Korea Kusini umewasili kwenye uwanja wa majaribio ya nyuklia wa Punggye-ri, Korea Kaskazini, ili kukusanya habari kuhusu hafla ya kufungwa kwa uwanja huo, wakishirikiana na waandishi wa habari kutoka China, Russia, Marekani na Uingereza.

    Wizara ya muungano wa Korea Kusini imesema, Korea Kaskazini ilipokea orodha ya majina ya waandishi wa habari wa Korea Kusini na kuwaelekeza kusafiri mjini Wonsa, Korea Kaskazini, kutoka Seoul, kwa kuchukua ndege ya serikali.

    Hii ni mara ya kwanza kwa ndege ya serikali ya Korea Kusini kusafiri moja kwa moja nchini Korea Kaskazini baada ya kutokea kwa vita ya Korea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako