• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Semina ya Uzoefu wa Maendeleo ya China yafanyika nchini Madagascar

    (GMT+08:00) 2018-05-24 18:41:38

    Hafla ya ufunguzi ya Semina ya Uzoefu wa Maendeleo ya China ya mwaka 2018 imefanyika Antananarivo, mji mkuu wa Madagascar na kuhudhuriwa na watu mbalimbali akiwemo Balozi wa China nchini humo Bw. Yang Xiaorong na mkuu wa ofisi ya Sekretarieti ya taifa inayoshughulika ushirikiano na maendeleo ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Madagascar Bw. Maminjatovoniaina Desire .

    Wanafunzi 53 kutoka idara mbalimbali za serikali ya Madagascar watajifunza uzoefu wa maendeleo ya China kwa wiki mbili.

    Bw. Desire amesema, anaamini kupitia semina hiyo, washiriki wote wataongeza zaidi ufahamu wao wa uzoefu wa maendeleo ya China na kuongeza imani yao ya matarajio ya ushirikiano kati ya Madagascar na China.

    Naye Balozi Yang amesema, serikali ya China imetoa misaada mbalimbali ya kiufundi kwa Madagascar chini ya ushirikiano wa nchi zinazoendelea, na semina hiyo itawawezesha watu wengi zaidi kujifunza uzoefu wa maendeleo ya China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako