• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wagonjwa wawili wa Ebola waliotoroka kwenye kituo cha tiba nchini DRC wakutwa wamefariki

    (GMT+08:00) 2018-05-24 18:44:46

    Mkuu wa Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) katika mji wa Mbandaka ulioko kaskazini magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC, Henry Gray amesema, wagonjwa wawili wa Ebola waliopotea wamefariki nchini humo.

    Dr Gray amesema, wagonjwa hao ni miongoni mwa watu watatu waliothibitishwa kuwa na maambukizi ya Ebola wiki iliyopita na walitoroka kutoka kituo kilichotengwa mjini Mbandaka siku chache zilizopita. Miili yao ilipatikana baadaye maeneo ya jirani.

    Katika siku za karibuni, wahudumu wa afya wameripoti wagonjwa kadhaa waliotoroka kutoka vituo maalum vilivyotengwa kuwahudumia wagonjwa wa Ebola.

    Wizara ya afya nchini DRC haijatoa kauli yoyote kuhusu vifo vya watu hao wawili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako