• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa wito wa kuheshimu uongozi wa Afrika katika kukabiliana na changamozo zinazoikabili sehemu ya Sahel

    (GMT+08:00) 2018-05-24 19:20:05

    Naibu balozi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Bw. Wu Haitao amesema, ili kukabiliana na changamoto zinazoikabili sehemu ya Sahel, jumuiya ya kimataifa inapaswa kuheshimu na kuonesha uwezo wa Bara la Afrika wa kujiamulia masuala yao wenyewe, na kuunga mkono juhudi za nchi na mashirika ya kanda hiyo katika kulinda amani na usalama kwenye sehemu ya Sahel.

    Bw. Wu Haitao amesema hayo kwenye Mkutano wa wazi wa vikosi vya muungano vya kundi la nchi tano za Sahel katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Amesisitiza kuwa inapaswa kuongeza nguvu kuunga mkono vikosi vya muungano, kuweka mkazo katika ufumbuzi wa kisiasa wa masuala muhimu yanayofuatiliwa, kuongeza fedha katika suala la kupambana na ugaidi kwenye sehemu ya Sahel, na kutilia maanani kazi ya mashirika ya kikanda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako