• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wizara ya ulinzi ya China yaeleza sababu za Marekani kufuta mwaliko wa China katika kushiriki luteka ya kijeshi ya Pasifiki

    (GMT+08:00) 2018-05-24 19:20:47

    Msemaji wa Wizara ya mambo ya ulinzi ya China Bw. Ren Guoqiang amesema, hivi karibuni Marekani limelifanya suala la Bahari ya Kusini ya China kuwa la kijeshi kwa kupotosha ukweli, na kukifanya kiwe kisingizio cha kufuta mwaliko kwa China kushiriki kwenye Luteka ya kijeshi ya pamoja ya Pasifiki ya mwaka 2018.

    Amesema uamuzi huo wa Marekani hauna maana ya kimkakati, na kufunga mlango wa kufanya mawasiliano hakusaidii kujenga uaminifu na kufanya ushirikiano kati ya majeshi ya pande hizo mbili.

    Bw. Ren Guoqiang amesema, China inatumaini kuwa Marekani itaangazia siku za baadaye na kushughulikia migogoro ipasavyo, ili kuufanya uhusiano kati ya majeshi ya nchi hizo mbili uwe chanzo cha kuhimiza utulivu wa uhusiano kati ya China na Marekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako