• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • "Hadithi kati yangu na Afrika" yaonesha ushirikiano wa kirafiki kati ya China na Afrika katika kipindi kipya

    (GMT+08:00) 2018-05-24 20:32:54

     Sherehe ya utoaji wa tuzo ya Mashindano kupitia mtandao wa Internet kuhusu "Hadithi kati yangu na Afrika" imefanyika leo hapa Beijing na kuwashirikisha watu takriban 200 wakiwemo watu waliopewa tuzo, mabalozi wa nchi mbalimbali za Afrika nchini China, pamoja na wanadiplomasia na wajumbe kutoka elimu na viwanda.

    Wajumbe hao wamejadili kwa pamoja urafiki wa jadi kati ya China na Afrika, na kufungua karne mpya kwa ushirikiano wa kunufaishana na kupata maendeleo kwa pamoja kati ya pande hizo mbili. Mashindano hayo yaliyoandaliwa na Sekretarieti ya Kamati ya utekelezaji wa miradi ya Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika na Radio China Kimataifa, yamekusanya makala, picha, na video kutoka nchi zaidi ya 46 barani Afrika. Mwalimu wa kujitolea kutoka Chuo cha Confucius katika Chuo Kikuu cha Cairo Bw. Huang Shuai amepewa tuzo ya ngazi ya juu kwa video inayosimulia uzoefu wake wa kutoa mafunzo kwa miaka miwili nchini Misri. Bw. Huang Shuai anasema:

    "Kusema kweli, sikufikiri naweza kupata tuzo ya kwanza, ninasisimka sana. Napenda sana filamu, hivyo natumia kamera kuweka kumbukumbu ya maisha ya kila siku. Video yangu ina mambo mengi niliyorekodi, ambayo inaweza kuwagusa majaji. "

    Mashindano hayo ni jukwaa la kuonesha ndoto za China na za Afrika, ambayo yamejumuisha picha na videio zinazohusisha sekta mbalimbali za ushirikiano kati ya China na Afrika, na kuonesha hadithi zinazohusu mawasiliano ya kirafiki na ushirikiano kati ya pande hizo mbili. Msaidizi wa Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Chen Xiaodong akihutubia kwenye sherehe ya utoaji wa tuzo anasema:

    "Makala hizo zimeonesha hadithi zinazogusa watu kati ya China na Afrika kupitia maandishi, picha na video fupi. Hadithi hizo zimejumuisha nguvu kubwa ya kuhimiza maendeleo ya ushirikiano wa kirafiki kati ya China na Afrika, na pia zimetutia moyo kuhusu siku za baadaye za uhusiano kati ya pande hizo mbili."

    Naibu mhariri mkuu wa Radio China Kimataifa Bw. Ren Qiang ameeleza kuwa, makala 42 zinazoshindania tuzo za ngazi tatu za mashindano hayo zimekusanya kura zaidi ya laki 2.5 kupitia mtandao wa Internet ndani ya siku 11, hali iliyoonesha upendo wa wachina na hamu kubwa ya kufanya ushirikiano kati ya pande hizo mbili. Bw. Ren Qiang anasema:

    "Shindano hili sio tu linawafanya wachina wengi zaidi kufahamu Afrika, bali pia linasaidia kuongeza hamu ya jamii ya China kufuatilia na kujiunga na ushirikiano kati ya China na Afrika. CRI inapenda kushirikiana na pande mbalimbali kuleta fursa nyingi zaidi kuhimiza mawasiliano kati ya China na Afrika. Tutashuhudia kwa pamoja mafanikio mengi zaidi yatakayopatikana kwenye maendeleo ya ushirikiano kati ya pande hizo mbili, mti wa urafiki wa China na Afrika utakuwa na ustawi mkubwa zaidi."

    Kuanzishwa kwa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika mwaka 2000 kulifungua ukurasa mpya wa ushirikiano wa kirafiki kati ya pande hizo mbili. Mwaka 2015, mafanikio ya mkutano wa kilele wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika uliofanyika mjini Johannesburg, Afrika Kusini, ulizindua njia mpya ya ushirikiano wa kunufaishana na kupata maendeleo kwa pamoja kati ya pande hizo mbili. Mwezi Septemba mwaka huu, mkutano wa viongozi wa Baraza hilo utakaofanyika mjini Beijing, utaweka mkazo katika ujenzi wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja", na kujenga kwa pamoja Jumuiya ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja, ambapo viongozi wa China na Afrika watajadili kwa pamoja mipango muhimu ya ushirikiano kati ya pande hizo mbili. Msaidizi wa Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Chen Xiaodong ameeleza kuwa, China na Afrika siku zote ziko katika jumuiya yenye mustakabali mpya, urafiki kati ya pande hizo mbili uko imara na umepata mafanikio mazuri kutokana na kuwa pande hizo mbili siku zote zinashikilia wazo la kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja, na kufungua ukurasa mpya wa ushirikiano wa kirafiki kati ya pande hizo mbili kwa kuchukua vitendo mbalimbali halisi. Bw. Chen Xiaodong anasema:

    "China na Afrika siku zote ni jumuiya yenye hatma ya pamoja. Chanzo cha urafiki kati ya China na Afrika kudumu na kuzaa matunda mengi ni kwamba pande hizo mbili zinaheshimiana na kuaminiana. Watu wa China na Afrika wanashikana mikono na kukabiliana na matitizo kwa pamoja, huku ushirikiano huo wenye usawa ukinufaisha pande zote. "

    Balozi wa Kenya nchini China Bw. Michael Kinyanjui aliyehudhuria sherehe hiyo anasema:

    "Kwanza, nataka kutoa shukrani kwa waandaaji wa shindano hilo, ambao ni pamoja na Chuo Kikuu cha Lugha na Utamaduni cha Beijing, Redio China Kimataifa na mashirika mengine. Kufanyika kwa shughuli hii sio tu kumewafanya washiriki kuonesha uhusiano wa ushirikiano wa kiwenzi kati ya China na Afrika kupitia jukwaa hilo, bali pia kumeimarisha mawasiliano ya utamaduni kati ya serikali na jamii."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako