Rais Paul Kagame amesema yeye kama shabiki wa klabu hiyo amefurahishwa na hatua hiyo .
Kagame amesema nembo hiyo itatumika kuvutia watalii Rwanda pamoja na wawekezaji wa kibiashara.
Afisa mkuu wa mauzo ya Arsenal Vinai Ventkatesham amesema wamechagua kushirikiana na nchi hiyo baada ya kurishishwa na mabadiliko ya maendeleo yake tangu tukio la vita.
Jezi ya Arsenal inatazamwa na watu milioni 35 kwa siku duniani na ni moja ya timu zinazopendwa sana na mashabiki.
Bodi ya maendeleo ya Rwanda imearifu kwamba Rwanda itaendelea kukuwa kiuchumi kutokana na mradi huo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |