• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Vladmir Putin wa Russia akutana na makamu rais wa China

    (GMT+08:00) 2018-05-25 10:04:44

    Rais Vladmir Puitin wa Russia amekutana na makamu rais wa China Bw. Wang Qishan ambaye yuko nchini Russia kuhudhuria Mkutano wa 22 wa Baraza la kimataifa la Uchumi mjini St. Petersburg.

    Kwenye mazungumzo yao, viongozi hao wawili wamekubaliana kuendelea kukuza ushirikiano wa pande mbili wa kunufaishana kati ya nchi zao.

    Bw. Wang amesema rais Xi Jinping wa China anazingatia uhusiano kati ya China na Russia, na anatarajia kukutana tena na rais Putin kupanga kwa pamoja maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili na Shirika la Ushirikiano wa Shanghai (SCO) ambalo litaitisha mkutano wa mwaka, mwezi Juni nchini China.

    Bw. Wang pia amesema viongozi hao wawili wametoa mchango mkubwa katika kukuza uhusiano wa pande mbili na kujitahidi kuendelea kusukuma mbele maendeleo ya uhusiano huo.

    Rais putin amesema uhusiano kati ya China na Russia umeendelezwa kwa kiwango cha juu katika nyanja zote. Pia amesema, Russia inapenda kuimarisha ushirikiano na China, kuongeza uungaji mkono katika mambo ya kimataifa na kuzidisha uhusiano wa wenzi wa kimkakati.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako