• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Argentiona yapata pigo baada ya kipa wake tegemeo kuumia mazoezini

    (GMT+08:00) 2018-05-25 08:39:39
    Timu ya Taifa ya Argentina imepata pigo baada ya kipa tegemeo, Sergio Romero kuumia akiwa anafanya mazoezi. Serigio alipata maumivu ya goti mazoezini juzi, siku chache kabla ya kuanza fainali za Kombe la Dunia Juni 14. Chama cha Soka Argentina kimesema Romero ameenguliwa katika kikosi hicho kwa kuwa majeraha yake yatachukua muda mrefu. Mchezaji huyo mwenye miaka 31 alicheza mechi nne za Man United za kuwania Kombe la FA kabla ya kuumia katika mechi za kimataifa. Kocha Jorge Sampaoli amebakiwa na makipa wawili Willy Caballero na Franco Armani. Argentina imepangwa Kundi D na timu za Iceland, Croatia na Nigeria.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako