• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kocha mpya wa Arsenal Unai Emery amesema anataka klabu hiyo iwe miongoni mwa klabu bora zaidi Ulaya.

    (GMT+08:00) 2018-05-25 08:40:37
    Kocha mpya wa klabu ya Arsenal Unai Emery amsema anapenda kuridisha hadhi ya klabu ya Arsenal barani Ulaya na duniani, na kuifanya iwe klabu yenye kuheshimiwa kama ilivyokuwa zamani. Mkufunzi huyo wa miaka 46 aliwatambulishwa rasmi kwa mashabiki na wanahabari Jumatano kabla yake, akiandamana na mmiliki wa Arsenal Ivan Gazidis. Arsenal walishindwa kufuzu kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya 2017 na wameshindwa kwa mwaka huu pia. Tangu mwaka 1998 walikuwa wanafuzu kila mwaka. Gazidis alisema Emery alikuwa kwenye orodha ya wakufunzi wanane waliokuwa wamewekwa kwenye mizani kumtafuta mrithi wa Arsene Wenger, lakini yeye ndiye aliyefaa zaidi. Wakufunzi wote wanane walishiriki usaili wa kina na hakuna hata mmoja aliyejiondoa kwenye mchakato huo. Kuwa Kocha wa Arsenal ni moja ya kazi nono kwa makocha duniani.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako