• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Iraq kuchunguza udanganyifu katika uchaguzi wa wabunge

    (GMT+08:00) 2018-05-25 09:18:23

    Serikali ya Iraq imeitisha mkutano kujadili tuhuma za udanganyifu na ukiukaji wa kanuni kwenye uchaguzi wa bunge uliofanyika Mei 12. Taarifa iliyotolewa na serikali ya Iraq inasema Baraza la mawaziri lilikutana na maofisa wa mahakama na ujasusi, na Kamati ya usalama ya Tume ya uchaguzi, kujadili usalama wa vifaa vya kielektroniki vilivyotumiwa kwa mara ya kwanza kwenye uchaguzi wa wabunge nchini humo. Taarifa inasema baraza hilo limeteua tume maalumu kuchunguza tuhuma za udanganyifu kwenye uchaguzi, na kuwasilisha ripoti kwa baraza hilo, baraza kuu la sheria na mahakama kuu, ili kutoa uamuzi kuhusu mchakato wa uchaguzi na matokeo yake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako