• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mjumbe maalumu wa UN atoa wito kurejeshwa kwa mazungumzo Burundi

    (GMT+08:00) 2018-05-25 09:42:12

    Mjumbe maalumu wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Burundi Bw Michel Kafando ametoa wito wa kurejeshwa kwa mazungumzo nchini humo baada ya nchi hiyo kurekebisha katiba yake kupitia kura za maoni.

    Bw. Michel Kafando amesema serikali ya Burundi inatarajiwa kuunga mkono kuanzisha upya mazungumzo shirikishi chini ya uongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Amesema kurejeshwa kwa mazungumzo hayo kunaweza kuwapatia warundi nafasi ya kujadili changamoto wanazokabili, na kusisitiza kuwa mazungumzo shirikishi ndiyo njia sahihi ya kupata ufumbuzi wa mgogoro wa sasa nchini humo.

    Ameonya kuwa licha ya kuwa kwa sasa hali inaonekana kutulia, mauaji ya hivi karibuni ya watu 26 yaliyotokea katika jimbo la Cibitoke, yanaonyesha kuwa bado hali sio ya utulivu. Pia amesema hali ya kibinadamu nchini Burundi bado inatia wasiwasi, huku warundi wakiendelea kuishi kwenye kambi za wakimbizi nchini Tanzania, Rwanda, Uganda na DRC.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako