• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la usalama la umoja wa mataifa lapitisha azimio kulaani njaa kama silaha ya vita

    (GMT+08:00) 2018-05-25 10:21:46

    Baraza la usalama la Umoja wa mataifa limepitisha azimio kulaani matumizi ya njaa kwa raia kama moja ya njia za vita. Muswada uliopendekezwa na Ivory Coast, Kuwait, Uholanzi na Sweden, unazitaka nchi mbalimbali kufanya uchunguzi kwenye nchi zao kuhusu ukiukaji wa sheria ya kibinadamu ya kimataifa inayohusiana na matumizi ya njaa kwa raia kama moja ya njia za vita.

    Kwa mujibu wa umoja wa mataifa sehemu kubwa ya watu wanaokabiliwa na tatizo la usalama wa chakula, na asilimia 75 ya watoto waliodumaa wenye chini ya umri wa miaka mitano wanaishi kwenye maeneo yaliyoathiriwa na migogoro, idadi yao ikikaribia milioni 74.

    Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limesema nchi 10 duniani ndizo zina msukosuko mkubwa wa chakula, ambazo ni Afghanistan, Burundi, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Iraq, Nigeria, Somalia, Sudan Kusini, Sudan, Syria na Yemen. WFP imelipongeza baraza la usalama kwa kupitisha azimio hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako