• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Afrika Kusini yachukua hatua kurekebisha makampuni ya kiserikali yenye matatizo

    (GMT+08:00) 2018-05-25 10:22:58

    Waziri wa Mashirika ya Umma wa Afrika Kusini Bw. Pravin Gordhan amefanya uteuzi wa bodi mpya za makampuni ya kiserikali ya Afrika kusini, ikiwa ni hatua ya kufanya marekebisho kwenye makampuni yanayoendeshwa vibaya.

    Teuzi zilizofanywa na Bw Gordhan ni pamoja na za mkuu wa Shirika la umeme la Afrika Kusini Eskom, Shirika la ndege la Afrika Kusini, Shirika la usafiri Transnet na Kiwanda cha kutengeneza silaha cha Denel. Akiongea baada ya mkutano wa baraza la mawaziri mjini Cape Town Bw. Gordhan amesema haya ni makampuni ambayo yamekuwa yakiendeshwa vibaya, na madhara yake yamekuwa yakiathiri sekta nyingine.

    Amesema utendaji mbaya wa makampuni hayo ulitokana na ufisadi na uendeshaji mbaya. Bw. Gordhan amesema hatua hiyo inatokana na utekelezaji wa hatua zilizotangazwa na Rais Cyril Ramaphosa kuhuru kurudisha utawala bora kwenye makampuni ya umma.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako